Habari
WAZIRI MKUU NCHEMBA ATEMBELEA UWANJA WA ARUSHA, AAGIZA WAFANYAKAZI KULIPWA KWA WAKATI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea uwanja wa Arusha ambao ni miongoni mwa viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika Mashindano ya Soka Barani Afrika(AFCON) 2027 kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
Amefanya ziara hiyo leo Aprili 17, 2026 ambapo amemtaka Mkandarasi na Wasimamizi wa uwanja huo kuhakikisha kila mtu anayehusika katika shughuli za uwanja analipwa na Mkandarasi atakayekiuka atafungiwa kufanya kazi Tanzania.
Aidha Waziri Mkuu Nchemba amesema ameridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo inaelezwa kuwa hiyo ni hatua kubwa ya uwekezaji uiiofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya michezo nchini.
