Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

TANZANIA KUTUMIA KONGAMANO LA KISWAHILI UFARANSA KUONGEZA WAZUNGUMZAJI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amesema Tanzania inatarajia kutumia Kongamano la Kimataifa la Kiswahili la nchini Ufaransa  kuongeza idadi ya wazungumzaji wa lugha hiyo ulimwenguni.

Msigwa amesema hayo Aprili 14, 2026 jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Said Othman Yakub, kujadili na kupanga mikakati ya kuhakikisha kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Julai 4 hadi 7,2026 linakuwa na mafanikio makubwa.

 Kongamano hilo  linalenga kuwa jukwaa la kimkakati la kuitangaza na kuibidhaisha  lugha ya Kiswahili barani Ulaya, na     linatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 kutoka sekta za elimu, uchumi, afya, kilimo, utamaduni na diaspora.