Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

TIMU

Ili kujua vikosi vya timu zingine zinazoshiriki michuano ya CHAN 2024 Bofya hapa

KIKOSI CHA TANZANIA KWENYE CHAN 2024

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi rasmi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kitakachoshiriki michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024.

Kikosi hicho kilichotangazwa na kocha Hemed Suleiman kinajumuisha wachezaji kutoka klabu kadhaa za Tanzania, zikiwemo Simba SC, Young Africans, Azam FC, Coastal Union, Singida Big Stars, JKT Tanzania, na timu ya vijana Ngorongoro Heroes.

Orodha Kamili ya Wachezaji Walioitwa:

Walinda Mlango:

  1. Aishi Manula (Simba SC)
  2. Hussein Masalanga (Singida BS)
  3. Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)

Mabeki:

  1. Shomari Kapombe (Simba SC)
  2. Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
  3. Mohamed Hussein (Simba SC)
  4. Paschal Msindo (Azam FC)
  5. Dickson Job (Young Africans)
  6. Wilson Nangu (JKT Tanzania)
  7. Abdulrazack Mohamed (Simba SC)
  8. Vedastus Masinde (U20 Ngorongoro Heroes / TMA)
  9. Lameck Lawi (Coastal Union)

Viungo:

  1. Ibrahim Hamad (Young Africans)
  2. Ahmed Pipino (U20 Ngorongoro Heroes / KMC)
  3. Mudathir Yahya (Young Africans)
  4. Yusuph Kagoma (Simba SC)
  5. Nassor Saadun (Azam FC)
  6. Jammy Simba (U20 Ngorongoro Heroes / KMC)
  7. Iddy Selemani (Azam FC)
  8. Sabry Kondo (Coastal Union)
  9. Feisal Salum (Azam FC)
  10. Sheikhan Khamis (U20 Ngorongoro Heroes / Young Africans)
  11. Clement Mzize (Young Africans)
  12. Mishano Michael (U20 Ngorongoro Heroes / Kengold FC)

Washambuliaji:

  1. Kibu Denis (Simba SC)
  2. Ibrahim Hamad (Tabora United)
  3. Abdul Suleiman (Azam FC) 

Tanzania inafuzu kwa mara ya tatu kwenye michuano hii. Kwa fahari na shauku ya taifa, Taifa Stars itajitahidi kufanya vizuri nyumbani ili kusonga mbele zaidi ya hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yake. Chini ya uongozi wa kocha mkuu Hemed Morocco, Tanzania italenga kunufaika na kupanda kwa ligi ya nyumbani na matokeo ya hivi karibuni katika mashindano ya CAF.