Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MHE. MWINJUMA AMTEMBELEA MWANAMUZIKI NGULI ZAHIR ALLY ZORRO, AMKABIDHI MSAADA WA MILIONI 10


 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, tarehe 8 Machi 2026 amemtembelea na kumjulia hali Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Zahir Ally Zorro, nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mwinjuma amemkabidhi Mzee Zorro kiasi cha Shilingi milioni 10 taslimu kama salamu za pole na faraja kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimtakia apone haraka.

Akizungumza baadaa ya kufika kumjulia hali, Mhe. Mwinjuma amesema Serikali inaendelea kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na wasanii wakongwe katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni wa Tanzania na kuwa wasanii hao ni hazina muhimu ya taifa, hivyo wanastahili kuenziwa na kupewa faraja wanapokumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya au kijamii.

Kwa upande wake, Mzee Zorro alitoa shukrani zake kwa Rais Samia pamoja na Serikali kwa upendo na kujali hali yake, akisema msaada huo ni faraja kubwa kwake na kwa familia yake katika kipindi hiki anachopitia.