Habari
NAIBU WAZIRI MWINJUMA AKUTANA NA WADAU WA MICHEZO NA BURUDANI KUJADILI FURSA ZA AFCON 2027
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa Sekta ya Michezo na Burudani jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
Vikao hivyo vilivyoofanyika kwa nyakati tofauti Machi 03, 2026, katika Ofisi ya Kituo cha Urithi wa Ukombozi, jijini Dar es salaam vimejikita katika kuandaa mazingira wezeshi yatakayowawezesha wadau hao kuwa sehemu ya mafanikio ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika inayotarajiwa kufanyika nchini.
