Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Maandalizi Tamasha la Nne la Utamaduni Kitaifa Yaanza

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza maandalizi ya Tamasha la Nne la Utamaduni Kitaifa ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti, 2026 Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya tamasha hilo tarehe 23 Julai, 2026  Jijini Dar es  Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Methusela Ntonda amesema, Tamasha hilo linalenga kuenzi  utamaduni wa Tanzania.

Amewataka waratibu wa Tamasha hilo kuhakikisha  linafanyika kwa ufanisi, akisisitiza kuwapo kwa mikakati ya kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa mafanikio.

slot gacor