Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MAKONDA: ACHENI KUFUATA TAARIFA ZA MITANDAONI, JIFUNZENI KUTAMBUA FURSA ZA KIUCHUMI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewahimiza Watanzania kuacha kuamini taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na badala yake kutumia programu za elimu ya fedha kuongeza maarifa ya biashara na uwekezaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Msimu wa Nne wa kipindi cha Elimu ya Fedha “Zogo Mchongo” uliofanyika Makao Makuu ya CRDB Bank jijini Dar es Salaam, Makonda amesema elimu ya fedha haiishii kuwaelekeza wananchi mahali pa kupata huduma za kifedha, bali pia huwafundisha namna ya kufanya biashara, kuendesha biashara kwa ufanisi na kutambua fursa zilizopo katika mazingira yao.

Aidha, amesema ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kifedha unalenga kuwapatia wananchi taarifa sahihi na maarifa yatakayowasaidia kufanya maamuzi bora ya kiuchumi na kujiongezea kipato.

slot gacor