Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MSIGWA AKOSHWA NA UBUNIFU WA BAJAJI ILIYOTENGENEZWA NA WANAFUNZI WA DIT


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amewapongeza Wanafunzi wa Taaasisi ya Teknolojia   Dar es Salaam (DIT) kwa ubunifu wa kuunda Bajaji inayotumia umeme.

Msigwa ametoa pongezi hizo alipotembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, maarufu Sabasaba leo Julai 08, 2026, na kuona bajaji hiyo katika banda la Taaaisisi hiyo.

Ameeleza kuwa, Serikali inawezesha Chuo hicho na kuwahimiza vijana kuendeleza bidhaa hizo za Teknolojia kuwa nzuri zaidi sokoni  na kuhimiza wakufunzi kuwasismamia na kuwatia moyo  Vijana hao katika kuendeleza ubunifu huo.

slot gacor