WIZARA NA UNESCO KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUHIFADHI URITHI WA UTAMADUNI
WIZARA NA UNESCO KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUHIFADHI URITHI WA UTAMADUNI
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni imeendelea kuimarisha ushirikiano na UNESCO katika kuhifadhi urithi wa utamaduni nchini, pamoja na kukamilisha nyaraka za uteuzi wa vazi la Kanga kama utambulisho wa Mtanzania na urithi wa utamaduni. Hayo yamejiri wakati wa kikao kati ya Idara hiyo na UNESCO kilichofanyika tarehe 18 Februari 2026 Mtumba Jijini Dodoma ambapo walijadili mwongozo wa kitaifa wa kulinda urithi wa utamaduni usioshikika. NITAFSIRIE IN ENGLISH Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, Jijini Dodoma kikijumuisha wataalamu kutoka Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Sanaa, Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini pamoja na Mtaalamu wa Utamaduni kutoka Ofisi za UNESCO Dar es Salaam. Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Bw. Boniface Kadili aliushukuru uongozi wa UNESCO Dar es Salaam kwa kuendeleza ushirikiano na Wizara katika sekta ya Utamaduni hasa katika uhifadhi wa urithi wa utamaduni pamoja na kutangaza lugha ya Kiswahili kimataifa.
