Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MHE. MWINJUMA ASHIRIKI USIKU WA MSWAHILI BURUNDI


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwijuma, ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Usiku wa Mswahili uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi, ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazoendelea kuelekea kilele cha Maadhimisho ya tano ya Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU 2026).

Mhe. Mwijuma ameshiriki katika tukio hilo akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. James Millya .

Usiku wa Mswahili uliwakutanisha viongozi wa serikali, washiriki wa Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kiswahili, wasomi, wabunifu wa sanaa na wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.

Tukio hilo lilipambwa na maonesho ya utamaduni, muziki na sanaa za Kiswahili, yakilenga kuenzi urithi wa Waswahili, kuimarisha mshikamano wa mataifa ya Afrika Mashariki na kuendelea kukuza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano, utamaduni, diplomasia na maendeleo katika ngazi ya kikanda na kimataifa.

slot gacor