Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

NAIBU WAZIRI MWINJUMA ATOA KAULI KWA WAZAZI NCHINI


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, amewataka wazazi na walezi nchini kusikiliza, kutambua na kuwekeza katika vipaji vya watoto wao na kusisitiza kuwa jukumu la mzazi si kumchagulia mtoto atakachokuwa, bali kumsaidia kuwa bora katika kile anachoweza kufanya.

Amesema hayo  leo Agosti 16, 2026, katika Mahafali ya 11 ya Darasa la Saba ya Shule ya Royal Elite,  yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.

Mhe. Mwinjuma ameeleza kuwa kila mtoto ana uwezo au kipaji cha kipekee ambacho kinapaswa kutambuliwa na kuendelezwa ikiwa  sambamba na elimu ya darasani.

“Mtoto akisema anapenda mpira, msimwambie moja kwa moja kwamba huo ni mchezo tu. Mtoto akisema anapenda kuimba, msimkatishe tamaa. Mtoto akionyesha kipaji cha sanaa, msaidieni kukiendeleza” amesema Mhe. Mwinjuma.

Aidha, amesisitiza kuwa kulea kipaji hakumaanishi mtoto kuacha masomo, bali wazazi wanapaswa kumsaidia mtoto kuwa na elimu pamoja na kipaji, akieleza kuwa mtu anaweza kuwa msomi na wakati huo huo akawa Mwanamichezo, Msanii au Mbunifu 

Pamoja na mambo mengine, ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza
wazazi kuwa chanzo cha hamasa kwa watoto kwakuwa wakati mwingine mtoto huhitaji msaada mkubwa kutoka kwa mzazi zaidi ya kusikia akiaminishwa kuwa anaweza kufanikiwa.

slot gacor