Habari
DIAMOND PLATNUMZ AZURU BANDA LA WIZARA YA HABARI SABASABA
Mwanamzuki Nyota wa Tanzania, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz, amepata nafasi ya kutembelea Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) kuona wizara inavyotoa huduma na elimu kwa wananchi.
Mwanamuziki Diamond ametembelea banda hilo leo Julai 11, 2026 kufuatia mwaliko wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).
