Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MKURUGENZI KANJE: MAFUNZO YAWASAIDIE KUTENGENEZA MAUDHUI YA KUWAPA HELA


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Kelvin Kanje amewataka Watengenza Maudhui walioshiriki mafunzo kwa awamu ya kwanza kutumia mafunzo hayo kuboresha kazi zao ili ziwaingizie kipato.

Amesema hayo Aprili 8, 2026 Jijini Arusha wakati akiwashukuru watengeneza maudhui hao kwa kushiriki mafunzo kwa awamu ya kwanza, akiahidi kuwafikia watengeneza maudhui katika mikoa mingine.

"Kwa wale mnaoanza mafunzo haya yatawasaidia kuinuka na wale ambao tayari mmeanza mfanye vizuri zaidi" alisema Bw. Kanje

Kwa upande wao washiriki wameshukuru kupata mafunzo hayo, wakisema yamewasaidia kuongeza ujuzi kwenye kazi hiyo, huku wakishauri yawe yanafanyika mara kwa mara.

Mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yamefanyika katika mikoa mitatu ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza, yakiwa na mada mbalimbali ikiwamo Kubiasharisha maudhui ya kitalii na kutengeneza kazi zenye matokeo, Mambo ambayo Taasisi za Fedha yanazingatia kabla ya kutoa mkopo na elimu ya kodi.