Habari
DKT. MWIGULU NCHEMBA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA AFCON
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mashindano ya AFCON, leo Jumatatu, Julai 27, 2026, ameongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo.
Aidha, kikao hicho kimewakutanisha viongozi kutoka wizara, taasisi mbalimbali za kisekta pamoja na mikoa itakayokuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027.
