Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

GWIJI WA SOKA RIO FERDINAND AELEKEA DODOMA KWA SGR


Gwiji wa soka duniani, Rio Ferdinand, ameendelea na ratiba yake hapa nchini ambapo leo Mei 20, 2026 ameelekea jijini Dodoma  kwa usafiri wa Treni ya Kisasa ya SGR kwa ajili ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na  vivutio mbalimbali vilivyopo katika jiji hilo.

Katika safari hiyo ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na ujumbe alioongozana nao.

Ziara hiyo inajumuisha pia kufanya mahojiano maalumu yanayogusia fursa mbalimbali za maendeleo ya soka nchini, ikiwemo uwekezaji, programu za vijana, na namna Tanzania inaweza kunufaika zaidi na uzoefu wa kimataifa katika kukuza vipaji.

slot gacor