Habari
MAKONDA ATOA WITO HUDUMA KUTOLEWA BILA UBAGUZI KAMBI YA KALOLENI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Paul Makonda, amewapongeza Madaktari, Wauguzi na Watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Kaloleni kwa kutoa huduma bora, huku akiwasisitiza kuendelea na huduma hiyo bila ubaguzi.
Makonda ametoa wito huo Mei 15, 2026 alipotembelea hospitali hiyo na kuzungumza na wananchi wanaopata huduma kupitia kambi ya matibabu inayofanyika hospitalini hapo na kusisitiza kuwa, kila mwananchi anayefika katika kambi hiyo anapaswa kupatiwa huduma.
“Hakikisheni hakuna mwananchi anayerejea nyumbani bila kupata matibabu anayostahili,” amesisitiza Makonda.
Ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuongeza upatikanaji wa huduma bora na za kisasa.
Kwa upande wao, wananchi waliojitokeza katika kambi hiyo, wakizungumza kwa wakati tofauti wamepongeza huduma zinazotolewa pamoja na ujio wa waziri Makonda ambao umeongeza faraja na kwao.
#AfyaKwaWote #Arusha #Kaloleni #Tanzania #SamiaSuluhuHassan
