Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MAKONDA- SERIKALI ITAENDELEA KUUNGA MKONO MATUKIO YA MICHEZO


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amesema Serikali itaendelea kuunga mkono matukio makubwa ya michezo kwa kuwa ni chachu ya ukuaji wa uchumi, kukuza utalii na kuibua vipaji vya vijana nchini.

Makonda amesema hayo wakati wa mbio za Cape to Cairo Arusha leo Mei 31, 2026.

Mbio hizo za kimataifa zimewakutanisha wakimbiaji kutoka Tanzania na mataifa mengine duniani katika mbio za kilomita 42, 21, 10 na 5. Lengo kuu ni kuhamasisha afya, kuendeleza michezo na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii wa michezo barani Afrika.

slot gacor