Habari
WAZIRI MAKONDA ATOA SALAMU ZA POLE MSIBA WA LUKUVI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Marehemu Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Ametoa salamu hizo Machi 28, 2026 wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo kinachofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katika salamu zake, amesema anaungana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Watanzania wote kuomboleza msiba huo mkubwa, akieleza kuwa taifa limepoteza kiongozi muhimu aliyetoa mchango katika taifa.
Waziri Makonda amesisitiza kuwa, marehemu Lukuvi atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka, uzalendo na mchango wake katika kuimarisha mifumo ya serikali na huduma kwa wananchi. Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuombea marehemu na kushikamana na familia katika kipindi hiki cha majonzi, akibainisha kuwa, maisha ya mwanadamu ni mafupi anapaswa kuishi kwa kuacha alama ya mema.
