Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

WAZIRI MAKONDA AMALIZA MBIO ZA KM 5 KILI MARATHON 2026


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Christian Makonda, ameshiriki na kufanikiwa kumaliza mbio za kilomita 5 katika Kilimanjaro International Marathon 2026 iliyofanyika Moshi. Ushiriki wake unaonyesha kuunga mkono jitihada za kukuza michezo, afya na ustawi wa jamii kupitia matukio ya kimataifa.

Tukio hilo limeendelea kuvutia washiriki na mashabiki kutoka ndani na nje ya nchi, likiimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha michezo na utalii barani Afrika.