Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

WAZIRI MAKONDA AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA SSEBO MIKOCHENI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda leo amefika katika Kanisa la Mtakatifu Martha kuungana na familia, ndugu na marafiki katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Biashara wa EFM na EATV marehemu Dennis Busulwa maarufu kama Ssebo.

Ibada hiyo imefanyika Parokia ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa sekta ya habari pamoja na wafanyakazi wa vyombo hivyo vya habari wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu, wakikumbuka mchango wake katika maendeleo ya tasnia ya utangazaji nchini.