Habari
WAZIRI MAKONDA AAHIDI MILIONI 20 KWA AFISA MICHEZO ATAKAYEFANYA VIZURI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda ameahidi zawadi ya shilingi Milioni 20 kwa Afisa Maendeleo ya Michezo ambaye atafanikiwa kuwa na michezo 20 inayofanya vizuri kwenye Wilaya yake.
Makonda amesema hayo leo Machi 28, 2026 wakati akifungua Kikao kazi cha 16 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo, kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha, huku akisisitiza kuwa, hatua hiyo inalenga kufufua vipaji vya vijana na kuwawezesha kiuchumi na kuitangaza nchi Kimataifa.
"Ninawaelekeza kwamba, mwakani tutakapokutana kila mmoja kwenye Wilaya yake awe na michezo angalau 20, atakayefanya vizuri tutampa zawadi na ataenda nayo nyumbani kwake", zawadi hiyo itakabidhiwa kwenye kikao cha 17 pamoja na Wizara kumtambua mshindi huyo alisema Makonda"
