Habari
WIZARA YA HABARI TUPO CHINANGALI KUTOA HUDUMA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutoa elimu na huduma za Sekta za Wizara hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yameanza leo Juni 16, 2026 katika eneo la Chinangali Park jijini Dodoma
Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni usajili wa wasanii na vikundi vya Sanaa, Udahili wa Wanafunzi kwenye chuo cha Maendeleo ya michezo Malya, kudahili Wanafunzi kwenye chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) kusajili Waandishi wa Habari kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.
Vile vile, Baraza la Michezo la Taifa linatoa elimu na kusajili vyama mbalimbali vya michezo.
Aidha, Michezo ya kitamaduni kama vile bao, drafti na karata ni michezo ambayo ni kivutio kikubwa katika banda hilo.
