Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MSIGWA: WIZARA YA HABARI NDIO MTIMA WA TAIFA


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema sekta za wizara hiyo, ndio mtima wa Taifa kwakua zinashikilia Utambulisho wa Taifa.

Amewataka Maafisa Utamaduni, Sanaa na Michezo kufanya kazi kwa ari, umoja na ushirikiano katika kusimamia Utamaduni na maadili ya Mtanzania.

Msigwa amesema hayo wakati akifunga Kikao kazi cha 16 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo, Machi 30, 2026 Jijini Arusha.

"Sekta hizi ndio zinasimamia Utambulisho wa Mtanzania hivyo Maafisa Utamaduni mnatakiwa kuonesha umuhimu wa kuwepo kwenu kwenye jamii kwa kuendeleza michezo, vipaji na kusimamia maadili", amesema Msigwa.

Pamoja na hayo, Msigwa amewataka kuwasilisha mawazo na Changamoto pindi wanapokwama ili wizara iweze kufanyia kazi.