Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI KIWANDA CHA UCHAPAJI (TSN)


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo  imeoneshwa kurudhishwa  na mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha uchapaji inaoendelea  katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambao  umefikia Asilimia 71.

Kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake  Mhe. Husna Sekiboko wakati wa ziara hiyo  katika  kampuni hiyo wamepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda ambaye ameeleza kuwa mradi huo unalenga kupanua uzalishaji wa biashara ya uchapishaji,  na kuwezesha kampuni kujitegemea na kutoa gawio kwa Serikali.

Kiwanda hicho ambacho  kitakuwa na mashine  18   ambapo kwa sasa zimeshafungwa   kwa asilimia  85 kinatarajiwa kuwa na  uwezo  mkubwa zaidi na kufanya vyema katika ushindani wa biashara ya Uchapaji Sokoni.