Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UKARABATI UWANJA WA UHURU NA MKAPA


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya michezo hususani kwenye miundombinu ya Sekta hiyo katika maeneo mbalimbali Nchini ikiwa ni pamoja na Kujenga na kukarabati Viwanja vya Mpira.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Husna Sekiboko wamepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda imesema hayo wakati wa ziara yake  katika Uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo, Machi 14, 2026.

Mhe. Sekiboko amesema kuwa, ziara hiyo inalenga kuangalia hatua zilizofikiwa katika ukarabati wa viwanja hivyo, ambavyo vinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya miundombinu ya michezo nchini hasa kipindi hiki kuelekea michuano ya AFCON 2027.