Habari
MSIGWA AWAKABIDHI AZAM MILIONI 20 ZA GOLI LA MAMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa @gersonmsigwa, amekabidhi kiasi cha shilingi Milioni Ishirini (20,000,000/=) kwa timu ya Azam FC kama zawadi ya “Goli la Mama” kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Zawadi hiyo imetolewa leo tarehe 11 Aprili 2026 jijini Dar es Salaam kama pongezi kwa Klabu ya Azam baada ya kupata magoli walipocheza na timu za Maniema union kutoka nchini DR Kongo na Nairobi united kutoka nchini Kenya kwenye hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
