Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

RIO FERDINAND AKABIDHIWA JEZI NA HASHEEM THABEET KUIMARISHA USHIRIKIANO WA MCHEZO WA KIKAPU


Katika hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano wa michezo kati ya Tanzania na Uingereza, gwiji wa soka Rio Ferdinand amekabidhiwa jezi maalumu ya timu ya kikapu ya Dar City na Mchezaji wa timu hiyo ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabeet.

Tukio hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam liliashiria mwanzo wa ushirikiano mpana wenye dhamira ya kuendeleza mchezo wa kikapu nchini, kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya michezo, pamoja na kuunganisha wadau na taasisi za michezo kutoka Tanzania na Uingereza kwa kiwango cha kimkakati chenye tija.

Katika mazungumzo yao, Thabeet na Ferdinand walijadili mikakati ya kisasa ya kukuza vipaji kupitia programu shirikishi, kuimarisha miundombinu ya mafunzo na matumizi ya teknolojia katika maendeleo ya wanamichezo. Pia walisisitiza umuhimu wa kujenga mifumo endelevu ya mafunzo, kliniki za michezo, na programu za kubadilishana uzoefu wa kimataifa ili kuwapa vijana fursa pana zaidi ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, aliunga mkono hatua hiyo akiitaja kama mwarobaini wa kuinua viwango vya michezo nchini kupitia ushirikiano wa kitaalamu na wa kimataifa. Aidha, alibainisha kuwa mpango huo utachochea fursa za kiuchumi kwa vijana, kuboresha mbinu za mafunzo, na kuufanya mchezo wa kikapu kuwa miongoni mwa nguzo muhimu za maendeleo ya michezo nchini.

slot gacor