Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

MKUTANO WA WADAU KUJADILI MKAKATI WA KITAIFA WA AFCON 2027


Wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali, serikali na sekta binafsi wameanza kuwasili katika hoteli ya Johari Rotana kwa ajili ya Mkutano Maalum wa Wadau wa kujadili Mkakati wa Kitaifa wa Maandalizi ya Mashindano ya AFCON 2027.

Mkutano huo unalenga kuweka mwelekeo wa pamoja kuhusu maandalizi ya Tanzania katika kushiriki na kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.