Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA KUWANUFAISHA WATENGENEZA MAUDHUI WA LUGHA YA KISWAHILI


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali imeanza mazungumzo na UNESCO pamoja na Uongozi wa Kampuni Mama inayomiliki Faceebok, Instagram na WhatsApp (META) ili Lugha ya Kiswahili itambulike rasmi kwenye Majukwaa ya Kimtandao na kuwezesha Vijana wanaotengeneza maudhui kwa lugha hiyo walipwe malipo makubwa kulingana na kazi zao.

Amesema hayo wakati wa Kongamano la 5 la Idhaa za Kiswahili duniani, linaloendelea jijini Arusha, leo Machi 24, 2026 ambapo amebainisha kuwa licha ya maudhui ya Lugha ya Kiswahili hususani ya Tanzania kuwa mazuri na kupata watazamaji wengi lakini warushaji maudhui hayo wanalipwa kidogo kutokana na lugha hiyo kutokuwa rasmi kwenye majukwaa ya mitandao hiyo ukilinganisha na Lugha ya Kiingereza,       

"leo hii unamkuta Mtu wa Tanzania ana followers zaidi ya milioni 3, akipost wanaotazama ni wengi ila hapati pesa kupitia Instagram, Facebook, TikTok hawawalipi kwasababu Kiswahili bado Watu wa META na wenye platform ya mitandao Duniani hawajakitambua kama lugha rasmi” alisisitiza Mhe. Makonda