Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

KONGAMANO LA 5 LA IDHAA ZA KISWAHILI


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akiongozana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, wakati akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), linapofanyika Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani, leo Machi 24, 2026.

Kongamano hilo la 5 la Idhaa za Kiswahili Duniani limeandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), likiwakutanisha wadau wa Idhaa za Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi linalofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Machi, 2026 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC), Jijini Arusha.