Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

LUGHA YA KISWAHILI KUFUNDISHWA NCHINI URUSI


Tanzania na Urusi zimekubaliana  lugha ya Kiswahili  kufundishwa katika Taasisi za elimu ya juu nchini Urusi, hii ikiwa ni jitihada za Serikali ya Tanzania kuhakikisha lugha hiyo inaongeza wazungumzaji na kuwa fursa ya ajira ulimwenguni.

Hatua hiyo imetokana na Kikao cha Tatu cha Tume ya pamoja ya Kimataifa ya Ushirikiano wa Biashara na Uchumi kati ya Tanzania na Urusi ambacho kimekutanisha Viongozi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali katika uchumi.

Akiongoza kikao hicho, Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo leo Mei 16, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha, amesema kuwa, Kiswahili kufundishwa nchini Urusi kitafungua fursa za kiuchumi na kuongeza wigo wa lugha hiyo kufahamika zaidi duniani.

Katika kikao hicho zoezi la utiaji saini mikataba mbalimbali ambapo Mkataba wa lugh ya Kiswahili kutumika kufundishia nchini Urusi umefanyika kati ya Mtendaji Mkuu wa Baraza la Kiswahili Taifa. Bi. Consolata Mushi na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi Bw.  Maxim Reshetnikov.


Pia amesema nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana  katika maeneo muhimu ikiwemo sekta ya viwanda ,kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, miundombinu ya usafirishaji na kuimarisha usafiri wa anga kwa kuanzisha usafiri wa ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda nchini Urusi.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda ameshukuru makubaliano hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kati ya Tanzania na Urusi kupitia sekta za wizara yake.

slot gacor