Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

.WAZIRI WA HABARI MAKONDA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2025/26 BUNGENI JIJINI DODOMA.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Kamati hiyo, chini ya Makamu Mwenyekiti Mhe. Cornel Lucas Magembe, imepokea na kujadili taarifa hiyo kama sehemu ya majukumu yake ya usimamizi wa shughuli za Wizara.