KIKAO CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI(PAC)
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Khalfan Hilaly Aeshi imepokea, kupitia na kuchambua taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa (TACAF).
Kamati imefanya uchambuzi huo tarehe 7 Agosti, 2026 Bungeni jijini Dodoma.
