Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

NAIBU WAZIRI MWINJUMA AAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO YA TAA UWANJA WA CCM KIRUMBA


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (Mwana FA), ameahidi kulifanyia kazi suala la changamoto za Taa katika Uwanja wa CCM Kirumba, kwa kushirikiana na wadau pamoja na wapenda maendeleo ya michezo nchini.

 Mhe. Mwinjuma ametoa ahadi hiyo Agosti 8, 2026 alipotembelea uwanja huo, ambapo amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inaboresha miundombinu michezo nchini.

"Moja ya changamoto kubwa iliyopo hapa Kirumba  ni ukosefu wa mfumo wa taa unaowezesha uwanja kutumika kwa ufanisi nyakati za usiku. Hali hiyo imekuwa ikipunguza fursa za kufanyika kwa baadhi ya shughuli za michezo, hususan mechi na matukio yanayohitaji matumizi ya uwanja wakati wa usiku, naahidi hili nitalifanyika kazi"Mhe. Mwinjuma.

Katika  ziara hiyo, Mhe. Mwinjuma ameambatana na Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, ikiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa, Abdul Mtua, ambapo wamepata fursa ya kuona hali halisi ya uwanja huo pamoja na changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili kuongeza matumizi na thamani ya uwanja huo kwa wananchi na wadau wa michezo.

Hatua hiyo inaendana na msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa kuendelea kuwekeza na kuboresha miundombinu ya michezo ili iwe katika hali bora, salama na iweze kutumika ipasavyo na wananchi pamoja na Wanamichezo.

slot gacor