Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

NAIBU WAZIRI MWINJUMA AWAKARIBISHA KANDA YA ZIWA KWENYE MIAKA 30 YA BONGO FLEVA


Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (Mwana Fa) amewakaribisha wananchi wa Kanda ya Ziwa wanaopenda burudani kwenye   Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva  litakalofanyika baadae leo tarehe 8 Agosti, 2026 katika ukumbi wa The Climax, Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ukaguzi  wa maandalizi ya Tamasha hilo, mapema leo Agosti 8, 2026, Mhe. Mwinjuma amesema Bongo Fleva ina historia kubwa katika tasnia ya muziki nchini, hivyo tamasha hilo linapaswa kuakisi thamani, historia na maendeleo ya muziki huo kwa miaka 30.


“Bongo Fleva ina historia yake na tunataka shughuli hii iakisi historia hiyo. Tunataka watu waje kuburudika na kupata burudani yenye ubora,” amesema Mhe. Mwinjuma.

Aidha, amesisitiza kuwa waandaaji wanapaswa kuzingatia uwezo wa eneo la tamasha ili kuhakikisha usalama wa mashabiki akieleza kuwa, ulinzi utakuwa wa kutosha.

“Maandalizi yamefikia asilimia 99. Leo tunachana kweli,” amesema Mhe. Mwinjuma.

Kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Hamad Ally (Madee), amewakaribisha wananchi waliokata tiketi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha hilo, linalolenga kutoa burudani bora na kuadhimisha safari ya miaka 30 ya Bongo Fleva.

slot gacor