Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

UWANJA WA BENJAMIN MKAPA NI KICHOCHEO CHA UCHUMI WA TAIFA


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa umekua unachochea mzunguko wa uchumi wa wananchi wa Temeke na Taifa kwa ujumla kupitia matukio ya kitaifa na Kimataifa ya kimichezo na kijamii yanayofanyika uwanjani hapo.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mhe. Mariam Nassoro Kisangi leo Aprili 20, 2026 Bungeni jijini Dodoma, ambapo amesema, kuwepo kwa uwanja huo katika Manispaa ya Temeke, kumeifanya kuwa kitovu cha michezo kitaifa na kimataifa na kuongeza heshima kwa nchi.