Habari
WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI WAUNGANA NA WENZAO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI
Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wameungana na Wafanyakazi wengine Duniani kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) mwaka 2026, yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ambapo kauli mbiu ni "Kazi zenye staha ni Nguzo kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050"
