Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Habari

SERIKALI YASISITIZA UJENZI WA ARENA KUBWA YA KISASA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ina mpango wa kujenga arena kubwa ya kisasa itakayokuwa kitovu cha matukio mbalimbali ya michezo na burudani nchini.

Akizungumza usiku wa kuamkia Julai 31 2026 wakati  tamasha la mchezo wa Masumbwi “Knockout ya Mama Season 9” liliofanyika katika ukumbi wa The super Dome  Masaki jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu  Nchemba amesema, Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza vipaji vya vijana kupitia uwekezaji katika sekta ya michezo na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.

Amesitiza  kuunga mkono juhudi za vijana na wadau wa michezo nchini, huku Serikali ikiendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha maendeleo ya michezo na kuibua vipaji.

slot gacor