Habari
MWINJUMA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA UGANDA KUJADILI MAANDALIZI YA AFCON
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, ameongoza Ujumbe maalumu wa Kamati ya maandalizi ya AFCON 2027 kutoka Tanzania ambao umewasili nchini Uganda, jana Aprili 21, 2026.
Ujumbe huo unatarajiwa kushiriki katika mkutano unaowakutanisha wajumbe wa kamati tatu za maandalizi za nchi wenyeji yani Tanzania, Kenya na Uganda ikiwa ni miongoni mwa juhudi za pamoja za kuhakikisha maandalizi ya AFCON 2027, yatakayofanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 18, 2027, yanaenda kwa kasi na kwa ubora unaokidhi viwango vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
