Habari
RAIS WA NAMIBIA MHE. DKT.NETUMBO ATEMBELEA NA KUPANDA MTI MJI WA SERIKALI MTUMBA
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah ametembelea kiwanja cha Ubalozi wa Namibia kilichopo katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma na kupanda mti wa kivuli katika eneo hilo.
Amefanya ziara hiyo, tarehe 21Juni, 2026 ambapo amepokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Katika Mji wa Serikali, Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah amepata maelezo kuhusu historia ya Mji wa Serikali ambayo yametolewa na viongozi na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo.
