Habari
TANZANIA MWENYEJI MISS WORLD 2027
Katibu Mkuu wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Gerson Msigwa pamoja na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Kampuni ya Miss World Limited Bi. Julia Morley wakisaini Mkataba wa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya 74 ya Ulimbwende wa Dunia mwaka 2027 (Miss World 2027).
Hafla ya utiaji saini mkataba huo, imefanyika Aprili 20, 2026 Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda.
