Habari
ALICHOKIFANYA MSIGWA YANGA DAY
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, ameshiriki katika Tamasha la Siku ya Mwananchi 2026 (Yanga Day) lililofanyika Agosti 9, 2026 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo, Bw. Msigwa alishiriki katika mchezo wa hisani uliowakutanisha wachezaji wa zamani pamoja na wafanyakazi wa Yanga dhidi ya timu ya wasanii wa filamu na muziki nchini.
Ushiriki huo umeonesha umuhimu wa michezo katika kuwaunganisha viongozi, wanamichezo, wasanii na wananchi, huku ukitoa nafasi kwa wadau mbalimbali kutumia michezo kama chombo cha kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano katika jamii.
Tamasha la Siku ya Mwananchi 2026 limekuwa pia jukwaa muhimu la kuendeleza uhusiano kati ya sekta ya michezo, sanaa na jamii, kupitia burudani na shughuli mbalimbali zilizowakutanisha wadau na mashabiki wa Klabu ya Yanga.
